(Translation in Swahili: Libère Tumba Mwanakalumbu)
Chupa katika bahari.
Chupa hii inaweza kuwa ni mjumbe wa kuangamia kale baharini, ambae anatujulisha siri. Lakini kweli kawaida ni salio la uchafu tu, plastiki, bila faida kubwa tunafikiri. Mwishoni wa mwenendo ulio onesha kuzaliwa kwake, akitengenezwa, kutumikia, kiisha kufadhaika, alifwata njia ya masalio yetu, kutokea kontena mbalimbali pamoja na vinginevyo. Mpaka siku ile, kugeukia maisha marefu walio mtakia ya muda wa miaka elfu (sio matumaini ya umri wa kuishi kwa plastiki!), alinaswa na nguvu za bahari, kutupwa huku na huku na mawimbi, hata kuishia katika nafasi hii ya kusangaza ambamo vipande vipande vingi vinayo hadithi kulinganishwa na yake, walimpokea chini ya jua zaifu. Haya, leo sasa yeye anaharibika katika uwasiliano na mahali za maji, akiambukiza punde kwa punde maji na mazingira. Na wakati mwili wake huaribika kwa vita za mawimbi na upepo, chupa hukumbuka …
Yeye kajiona katika ghorofa alimo pelekewa siku moja, akipita mkono kwa mkono katika undugu usiyotarajiwa hata kumpa kizunguzungu kifupi na kisicho fananishwa. Alikuwa hivyo na kiburi, tokeo la kazi la wanadamu, tajari kutumiwa. Hakutengenezwa kwa hayo?! Ndiyo, chupa linakumbuka kuzaliwa kwake katika kampuni, sawa vile angeliweza kujivunia mamlaka ya maendeleo ya kiufundi iliyo mruhusu kuleta ustarehe na ustawi wa watumiaji wake, akishirikia mwenendo mkubwa wa kiuchumi muda wetu.
Bila shaka katika suala hili, na ingawa yeye hakuwa mtaalam, akasikia wamoja wakiongelea ukosefu (mgogoro) wa fedha, ongezeko la joto duniani, vitisho kwa mazingira, hatari kwa maisha ao kwa afya. Lakini haya yote yalionekana kua mbali, hivyo giza huko mbele ya hiki chombo kikubwa na kizuri cha wakati wetu ambacho yeye alikuwa mmoja wa warithi! Hakuwako yeye kama alama ya usimamizi/utawalo wetu wa umeme/nishati, hasa wa mafuta! Hakuwako yeye aliyetoa maana kwa matunda ya mlimo aliokuwa na haki ya kuibeba ndani mwake kwa faida ya chakula! Hata akiwa akijishusha, hata matumizi yake kupangiwa kwa muda, chupa hujikumbusha jamii hii ya matumizi ambayo alipatikania wakati muda, akikamilisha nafasi yake katika mpango wa mambo aliowazia utawala unao kamilika, hatimaye, kadiri vile « chupa » anaweza kudhania. Hata Rafiki moja akamuhadithia hadithi ya kijana huyu aliyekua na matatizo ya kuendelea kutembea, aliyeweza kushinda kilema chake, akichukua mfano pia kutimiza pamoja na marafiki wake, kibano kimoja walicho kichapa katika vipimo vitatu, kwa kumruhusu pia kufungua chupa kama wao. Ajabu!
« Chupa », tazameni jina moja! Yeye hapa akijiuliza jinsi gani hutamkwa jina hili katika lugha za dunia. Jina hili ni la kike ama la kiume? Upande wowote labda? Lugha nyingine, akifikiria wakati huo kwa mara ya kwanza, bado hawajui jina hili ao hawakulijua zamani… Hiyo huwa shida kidogo kwake. Namna gani kujaza upungufu huo? Ni hapa anachugua ufahamu kwamba uteuzi wake uliweza kumpa sio tu maana na sura, lakini ulishirikia katika utambulisho wake … Je yeye atakua hivi na nafasi katika kamusi ya wakati wetu? Bila shaka! Afikirivyo akijaza kifua. Je, yeye si ni katika jamii nzima uvumbuo mkamilifu wa kisasa, akijichugulia mwenendo wa mbele, maendeleo?
Tazama, kwanza mshangao, sababu wakati unao zungumuziwa maendeleo, yeye anadhania anona ndege isio mtembezi ndani kuruka juu ya nafasi ambapo alipo… Ndege isio mtembezi ndani, katika kona/nafasi hii iliotelekezwa? Ni udanganyifu, bila shaka. Chupa husema basi yeye alibidi kuvurugiwa na hurudilia mwendo wa kufikiri fikiri kwake.
Kama angeliweza kuandika vitabu, angelihadithia bila kuchoka mahali pageni alioweza kupita na kuvuka munamo bara na bahari, katika mito, milima, pori na miji. Wengi watashangaa, kwa sababu chupa alivuka mipaka mingi, nchi nyingi … akitambua wazi madaraja ya kukosa usawa, ya utajiri, ya umaskini bali pia utawanyaji wa biashara na tamaduni ambako uchafu haubaki tofauti! Nani hujua, labda anaweza hata kusaidia kufafanua maonyo yetu ya dunia, chupa za plastiki zikipata sana matumizi kadhalika, zikionyesha vipaji visivyomalizika vya watumiaji wao!
Kumekuwa muda mrefu, wakati mfano wake wa kwanza umechorewa kunako meza ya kazi ya mhandisi, ndani ya uzuri wa aina yake, na mupaka wa mikunjo ya wembamba wake, chupa angelikuwa karibu kuapa kuweza kuushinda ulimwengu. Ujio ulikua wake. Hatari yoyote haikukaribia mawazo yake, na aina yoyote ya ajali ilionekana hivyo mbali, hivyo isiowezekana… Ila tazama hata anajitambua leo sasa dhaifu, akihukumiwa kupoteza hali katika mahali ya maji isiyokua mahali mazuri ya kujisifia … Ni hivi chupa huanza kua na shaka. Je, angeliishi tofauti kama angelijua mbele ya wakati?
Yeye hapa akikumbuka udhaifu wa ulimwengu huu sawa mwenyi kuonywa uzidi wa hatari kwa vitu vyote kama yeye, pia aina zote namo pia uanadamu. Anajisikia ndani mwake, katika kila moja wa molekuli wake uvunjikao, kua vile ukomo wa historia, wa uguzi na pia kujiuliza kusioepukika. Yeye aliye tu chupa baharini, sasa hujiuliza katika nguvu yake ya mwisho, ni nini bado ya kutimiza na ya kuweza. Yeye hatimizi mkataba wake/sayini yake bila matumaini ya upya wake! Ni nani awezae kuchugua kipimo cha hali hii igeni?
Ndiyo chupa hujisikia bila tumaini sana peke yake. Angelipendelea kupasha ulimwengu anavyo jisikia, kuigusa dhamiri ya « sisi » walio macho, kwa matatizo mengi ya kisasa na uharaka wa jibu lao, lakini sio kwepesi kwa chupa lenyi kua likifia juu ya bara lisilo, lisilo bado. Hakika vizazi vijavyo hawatasikia kamwe kuhusu kusimuliwa kwake…
Angeliweza kutoa sana kwa kuweza kubadili hayo, ili kusaidia kuelewesha kwamba inafaa pengine kujifunza kukataa vitu fulani, kufikiria tena namna ya maadibisho yetu kwa vitu, kwa viumbe, kwa ulimwengu. Lakini akiangalia pembeni yake, yeye anaamini kufikiria kwamba hayo yote ni kama ndoto. Ndoto ya chupa – plastiki – baharini, ambayo haiweze tena kuamsha hukumu, wala kuzaa elimu yoyote. Haya, yametimia, maamuzi yamekamatwa… Hayupo nafasi njema kwa kututhabitisha haya! Basi chupa hujinenea kwamba yangelikua ya kurudilia kuyafanya tena … Kiisha kanyamaa kwa sababu yeye hujua kwamba haiwezekane kurudi tena nyuma. Kwa hiyo asema kwamba kama ingelikua ya kufanya, sherti kutangulia huu mchanganyo wote, mwangazani wa mgawanyo bora …
Ghafla chupa kanyamaa… Bila kujichungia, mkono moja ukamchukua… Naye anashindwa kuaminia, ijapokua hakuna shaka lolote, hata kasikia tena joto ya muungano ambayo iliyomupa upendo wa ulimwengu huu. Akiwa katika haraka ya mawazo kwa ghafla, yeye akaona picha ya maisha yake za tembea: michoro ya mhandisi, kupewa sura, kiwanda na pia kiwanda cha kupanga chupa, mimbali ya duka aliko nunuliwa, furaha kubwa ya ghorofa, njia alimopita kwa kuchuguliwa kama uchafu, na vipindi vyote vya njia isio kuwa waziwazi na iliyo mjulisha bahari pana! Na nihapo kasikia sasa sauti ambayo hakusikia tena kwa muda mrefu sana : « Tazama, atoka wapi yule!? » « Ajabu! Mfano mzuri, mchukue … «